25 Machi 2025 - 16:17
Wananchi wa Iran wanapaswa kutangaza utayarifu wao wa kuwasaidia wapiganaji wa Palestina kwa kushiriki katika maandamano ya Siku ya Quds

Katika kizingiti cha Siku ya Quds Duniani, Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom imetoa taarifa ikizitaka sehemu zote za Taifa pendwa la Iran kushiriki kikamilifu katika Matembezi ya Amani ya Siku hii ya Quds na kutangaza kwa mara nyingine uungaji mkono wao kwa Muqawamah (Upinzani) wa Kiislamu wa Palestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Jumuiya ya walimu wa Seminari ya Qom imetoa taarifa katika Kizingiti cha Siku ya Quds Duniani na kuzitaka sehemu zote za Taifa pendwa la Iran kushiriki kikamilifu katika Maandamano ya Amani ya Siku hii, na kwa mara nyingine tena kutangaza uungaji mkono wao kwa Muqawamah wa Kiislamu wa Palestina.

Taarifa hii inasema:

Siku ya Al-Quds ni Siku ya kuhuisha Umma wa Kiislamu na Maonyesho ya nguvu ya Umma wa Kiislamu. Ushiriki wa kuvutia na wa kishindo wa Taifa shujaa na Wapiganaji la Iran hususan vijana wenye bidii katika Matembezi ya Siku ya Quds Duniani ni kutangaza uungaji mkono kwa Wadhulumiwa wa Palestina na kufanya upya Mapatano (Ahadi) yetu na Marhumu Imam - Khomeini (RA) - katika kuendeleza mapambano dhidi ya - Uistikbari na - Ghururi ya Kimataifa na Uzayuni wa jinai.

Inatarajiwa kuwa makundi yote ya Taifa hili adhimu kwa mara nyingine tena yatatangaza uungaji mkono wao kwa Muqawamah wa Kiislamu wa Palestina kwa kushiriki kikamilifu katika Siku hii ya Kimataifa na kutangaza utayarifu wao wa kuwasaidia wapiganaji na wapambanaji, wana Muqawamah wa Palestina.

Bila shaka, hatua thabiti za Waumini waliofunga Siku hii ni jihadi kubwa katika vita dhidi ya Israel.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha